14-12-2022

Prezidenti wa Bunge alimpokea katika offisi yake ya kazi Kiongozi mkuu wa Shirika la CBCA

Katika muji mkuu Kinshasa Mchungaji Dk. Jonathan K. Kivatsi anaendelea na juhudi zake za utetezi kuhusu masuala yanayohusiana na hali ya kibinadamu mashariki mwa DRC, hasa katika Kivu Kaskazini na Ituri.

Kwa muktadha huu, ndiyo kwanza amekutana na namba 1 wa Bunge leo jumatano 14 decemba 2022, Mheshimiwa Mbosso katika katika offisi yake ya kazi pale Ikulu ya wananchi. Huyu alipongeza sana hatua zinazofanyika na CBCA katika eneo hili la nchi kwa sekta kadhaa (kiroho, kibinadamu, kijamii na kiafya) na kusema yuko tayari kuhusika kibinafsi ili kuunga mkono zaidi juhudi na mipango kadiri iwezekanavyo.

Katika maongezi haya, alipewa aliko kirasmi kwa kuhuzuria mkutano wakushimika rasmi viongozi wapya wa Shirika la CBCA uliopangwa mwezi wa tatu mwaka ujao.

 

Communication CBCA

0 commentaire(s)

Aucun commentaire pour l'instant...

Laissez un commentaire