23-12-2022

CBCA inahuzuni kubwa kutangaza habari ya kifo ya Waimbaji zaidi ya 15 wa kwaya Upendo ya CBCA Kyavinyonge

Kanisa letu la CBCA linahuzuni kubwa kutangaza habari ya kifo ya Waimbaji zaidi ya 15 wa kwaya Upendo ya CBCA Kyavinyonge waliozama katika ziwa (Lac) Edouard wakijielekeza kwa mkutano mkuu wa injili kunako CBCA Kisaka, eneo ya Lubero. Watu walikua karibu 24 kwenye mtumbwi.

Mpaka hapa watu 5 ndio wameokolewa. Zaidi ya watu 15 hawajaonekana bado. Tunaomba wakuu viongozi wa serkali kutusaidia kutafuta watu ao miili ya watu ambao bado hawajapatikana. Tunaomba pia viongozi kutusaidia kwa kadiri ya uwezo wao kwa ajili ya mazishi ya waliofariki.

Tunatoa pole kwa Kanisa la CBCA Kyavinyonge na jamaa zote ambazo zimekumbwa na msiba huu wakutatanisha. Kanisa letu la CBCA kwa ujumla lina uchungu mwingi sana kuwapoteza watumishi wengi hao waliokua katika safari ya kiinjili.

Mungu wetu ambaye ni Emanueli, Mungu pamoja nasi, atupe nguvu na faraja inayo faa katika kipindi hiki kigumu. Zaburi 46:1 inasema “Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, musaada utakaoonekana tele wakati wa mateso”. Tumukimbilie Mungu kwa wakati huu wa uchungu.

KWA NIABA YA ECC/3ème COMMUNAUTE BAPTISTE AU CENTRE DE L’AFRIQUE

Rév. Dr Jonathan KAVUSA KIVATSI

Président et Représentant légal

0 commentaire(s)

Aucun commentaire pour l'instant...

Laissez un commentaire