08-10-2026

UONGOZI WA KKKT–DAYOSISI YA KASKAZINI MASHARIKI WAMPOKEA MTHEOLOJIA ALEMBA BIN HERMAN

Uongozi wa KKKT–Dayosisi ya Kaskazini Mashariki umempokea Mtheolojia Alemba Bin Herman, kutoka kanisa la Baptist Church in Central Africa (BCCA), Himbi 1 Usharika wa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mtheolojia Alemba atakuwa katika Dayosisi yetu kwa kipindi cha mwaka mmoja kupitia mpango wa kujitolea wa UEM South to South Volunteer Programme, unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Dayosisi yetu na UEM (United Evangelical Mission).

Ujio wake unalenga kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu wa kitheolojia na kiutumishi, pamoja na kujenga mahusiano na kujifunza kwa pamoja kati ya makanisa wanachama wa UEM.

Uongozi unamtakia Mtheolojia Alemba Bin Herman kipindi chenye baraka, mafanikio na matunda mema katika huduma yake kwa kipindi chote atakachokuwa pamoja nasi.

North Eastern Diocese

Tags News

0 commentaire(s)

Aucun commentaire pour l'instant...

Laissez un commentaire