11-11-2023

CBCA: Viongozi wa Shirika wamewasili mjini Bukavu leo alhamisi 9 novemba 2023 kwa ziara ya kazi ya siku tatu.

Ni pamoja na Mch. Dkt. Jonathan K. Kivatsi, Prezidenti na Kiongozi mkuu wa CBCA akisindikizwa na makamu wake Mch. Martin Kilumbiro pia na Mkurugenzi anaye husika na fedha bwana Pascal Munoka ndio ujumbe mkubwa huu umewasili Bukavu leo hii siku ya nne kwa saa za mchana.

Katika ziara hii ya kazi, viongozi hawa wa Shirika wataweza kushimika rasmi Mchungaji mwangalizi mpya wa Poste Bukavu Dkt. MUNGUIKO Sébastien ambaye aliteuliwa siku zilizopita na kukubaliwa na Kamati ya Utendaji ya CBCA. Kazi hii itafanyika jumapili katika ibada kubwa kwenye Usharika wa CBCA Bugabo/Bukavu.

Ujumbe huu utajielekeza pia Muku kwa ajilitu ya kazi. Viongozi wengine wa ma idara mbali mbali watawasili hivi Karibuni katika mpango huo.

Daniel Muyisa B. [Communication CBCA]

0 commentaire(s)

Aucun commentaire pour l'instant...

Laissez un commentaire